SAKATA la Taasisi ya Kuweka na Kuvuna Pesa (DECI), limechukua sura mpya baada ya wanachama mbalimbali wanaodai fedha zao kuapa kumpigia kura mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMAA), Dk.Willibrod Slaa.
Mbali ya uamuzi huo, waathirika hao wakiwemo viongozi wao, wametangaza kumpigia kampeni Dk. Slaa kwa ndugu, jamaa na marafiki zao.
Vuguvugu la wana DECI limeibuka siku mbili tu baada ya Dk. Slaa kuahidi kulipatia ufumbuzi suala la madai yao yaliyotokana na kuwekeza fedha kwenye kampuni kisha kushindwa kuzipata.
Akizungumza na Tanzania Daima jana mjini Dar es Salaam, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Dharura ya wanachama hao katika ufuatiliaji wa fedha zao, Mchungaji Isack Kalenga, alisema suala la DECI ni kidonda kisichopona kwa wanachama kutokana na serikali kuwanyang’anya fedha hizo.
No comments:
Post a Comment