
Selemani Msindi a.k.a Afande Sele ambaye ni msanii kioo katika Muziki wa Bongo Fleva, amepigwa madongo ya kutosha na wadau wa mtandao mmoja wa burudani nchini.
Mtandao huo ulitundika picha ya msanii huyo akiwa amevua nguo jukwaani katika moja ya shoo yake ya hivi karibuni, jambo lililotafsiriwa na wachangia mada hao kuwa ni uchafu.
“Hivi anavyofanya siyo ishu kabisa, kwanini afanye mambo machafu kama haya tena jukwaani? Ni akili zake au bangi? Kama umekwenda na mtoto kwenye shoo hiyo anajifunza nini? Hapo kachemka vibaya sana,” mtoa maoni mmoja alisema.
Wadau hao wameonekana kukerwa na picha ile ya Afande ambayo inamuonesha akiwa amevua suruali na kubaki na nguo ya ndani (kama anavyoonekana pichani kushoto) ambayo inamshushia heshima.
Mmoja wa wachangiaji hao, alisema kinachomharibia Afande ni kuiga mambo ya kigeni ambayo kiasi siyo utamaduni wetu.
“Sele (Afande) anaweza muziki, sauti yake tu ni tiba tosha ya moyo, kwanini aanze kufanya mambo yasiyo na msingi? Anatakiwa kutulia na kuachana na mambo ya kuiga ambayo hayana maana yoyote zaidi ya kumshusha thamani mbele ya jamii,” alisema mdau huyo.
“Lakini wakati mwingine hawa mastaa wakishafanya kila kitu na kumaliza, wanakosa vitu vipya, kwahiyo wanajikuta wakifanya hata yale yasiyo na maana kwa ajili ya kusaka umaarufu, huku ni kutafuta umaarufu kwa njia ya mkato ambako mwisho wake siyo mzuru,” alisema mdau mwingine.
Afande Sele ni kioo cha jamii, ni dhahiri kwamba, wanaomzunguka wanapenda kujifunza kutoka kwake, kitendo cha kuvua nguo jukwaani siyo cha kiungwana na kwa hakika kinamshushia heshima msanii. -MHARIRI.
No comments:
Post a Comment