Blog Entry

Sunday, August 30, 2009

ETI ‘DECI’ YA UKAHABA






Katika kuthihirisha kwamba, serikali iko katika wakati mgumu wa kuwadhibiti akina dada wanaodaiwa kujihusisha na biashara haramu ya ukahaba ‘kuuza sukari’, warembo hao wamebainika kuanzisha genge lao ‘deci’ ya ‘bizinesi’ hiyo na sasa ni kimataifa zaidi.

Hivi karibuni gazeti la Ijumaa lilitonywa juu ya mbinu mpya ya machangudoa kujiunga katika mtandao mmoja unaomilikiwa na mbongo anayejulikana kwa jina moja la Mawazo ambao unawaunganisha makahaba hao na wanaume ulimwenguni kote hivyo kuwepo kwa uwezekano wa biashara hiyo kushamiri kwa kasi ya ajabu.

Uchunguzi wa Ijumaa umebaini kuwepo kwa wafadhilli wakubwa wa mtandao huo ambao kazi yao kubwa ni kufanya udalali kwa dada zetu nchini kwenda kwa vibosile wa ndani na nje ya nchi.

Katika harakati zao ndani ya biashara hiyo haramu inayofanywa kwa njia hiyo ya kisasa, vimwana hao wamekuwa wakitakiwa kutuma picha zao ‘seksi’ ambazo huingizwa mtandaoni kwa ajili ya kunadiwa kwa wanaume.

Aidha, wanaume wanaotembelea mtandao huo hukutana na picha za warembo mbalimbali wakiwa watupu ambapo mteja naye hutakiwa kujisajili ili awe katika nafasi nzuri ya kukutanishwa na kahaba atakayemvutia kwa malipo maalum.

Hata hivyo, mwanaume anapofanikiwa kukutanishwa na mrembo aliyevutiwa naye, hutakiwa kupiga picha akiwa anafanya mapenzi ambapo picha hizo huingizwa tena kwenye mtandao huo ili kuweza kuwavutiwa watu wengine.

Wanaume wanaojisajili na mtandao huo pia hupewa nafasi ya kutoa maoni yao juu ya huduma wanayopewa na warembo hao ili kumfanya mteja mwingine kuweza kufanya uchaguzi sahihi.

Katika nusa nusa ya Ijumaa ambalo nalo lilijiunga kama mrembo, kigogo aliyedhani anachati na changudoa ndani ya mtandao huo bila kufahamu kuwa alikuwa akijibizana na paparazi wetu, alijikuta akianika mambo yake binafsi akiamini kuwa, muda mfupi angekutana na mrembo mkali.

Mazungumzo kati ya mnusaji wetu na ‘mnene’ huyo ambaye alijitambulisha kuwa ni mfanyakazi katika moja ya migodi ya dhahabu nchini, yalibainisha kuwa, baadhi ya hoteli zenye majina makubwa nchini (majina tunayo) zimekuwa zikitumika katika kufanikisha uchafu huo.

“Nafanya kazi katika kampuni ya …(akitaja jina) ya madini, jana nilitembelea… (akitaja jina la hoteli), nilikutana na mwanamke mmoja mrembo katika Hoteli ya…(akitaja jina la hoteli maarufu jijini Dar iliyoko ufukweni mwa Bahari ya Hindi), mwembamba na akanivutia sana.
“Baada ya kukaa kwa muda wa sekunde 10 tu, aliniambia jina lake ni Monica na ana umri wa miaka 22, ni mwanafunzi wa chuo kimoja maarufu cha jijini Dar es Salaam.

“Asikwambie mtu mtoto alikuwa na bodi zuri, kila kitu kilikuwa kimepangiliwa vizuri, anaongea kwa ufasaha lugha ya Kiingereza.
“Tulikunywa kidogo na mara akaniongoza kuelekea katika moja ya vyumba vya hoteli hiyo ambapo nilikutana na warembo wengine ambao wamepanga vyumba mahali hapo.

“Huduma aliyonipa ilikuwa si ya kitoto, nilijikuta nikikubali kutoa dola 50 za kimarekani kwa huduma ya usiku mmoja,” ‘Chatingi’ iliishia hapo.

Imedaiwa kuwa, mtandao huo unawashirikisha warembo hao ambao ni watoto wa vigogo, medenti wa vyuo vikuu na majimama ya mjini ambao wanapoonekana mitaani hakuna anayeweza kuamini kama wanaweza kufanya hivyo.

Katika kuhakikisha kwamba, wahusika wanatambulika na kuchukuliwa hatua, gazeti hili limeamua kutumia picha za baadhi ya akinadadapoa hao wa kitanzania ukurasa wa mbele. Ijumaa linawaomba wanaharakati wanaowatambua akinadada hao kuwasiliana na gazeti hili linaloendelea kuchunguza ‘DECI’ hiyo ya ngono, ili kulinusuru taifa.

No comments:

Post a Comment